Salmin Swaggz - Vikwazo lyrics

Published

0 253 0

Salmin Swaggz - Vikwazo lyrics

[Verse 1] - Salmin Swaggz They say, napenda unavyochana kama Easy E Wananiuliza mtaani vipi mbona hatusikii I heard ulianza fanya rap 2003 Mi nna visions, you gotta be blind to see Niko makini sio beef za kiuswahilini So snitch...kaa mbali nami mi pesa pesa na mimi Bila pesa hakuna life...hutaki, kufa maskini Usiniblame Scandal chafu na matusi ya mwilini Enzi hizo sikuelewa maisha naispend pesa isokwisha Wajinga walishindwa bainisha life walitaka ipindisha Niko...duniani kama sielewi what's going on Baniani,fanani hatuachani...mabeef, Money n so on Kwa upeo na hizi akili mi ni dili So hili pini wan*liafiki wenye roho na wasio na mwili Mi ndo...sauti ya mtaa...bungeni huu ndo wasaa Chungeni izo bambataa...tutaachana kwenye mataa, holla! [Hook] - Chozi Nimeshaona mbele, now the game is right on Kuna vikwazo tele, jasho langu halivuji bure [Repeat] [Verse 2] - Salmin Swaggz Si mgeni kwenye Mitaa maskani imetoweka amani mfano wa... Mtoto wa nyumbani kuitangaza siri ya ndani Au kwa nchi ya ki-dictator na wapinzani wakiwemo ndani Fisadi naona unapeta ila usipime huku kitaani Fani naiendeleza maslahi hayatanipoteza Daima siwezi teleza mpaka naliona jeneza Ni ngumu hamuwezi kucheza, kwa waliojaribu kubeza Walishindwa kunipoteza...kwenye upenyo napenyeza...ah! Nafkiri mpaka nahisi stanza zinavuja Watu wanasubiri mfano wa basi linakuja Wanakejeli una siku mbili, kwanza umeshachuja Brother ana division 4 na paper imevuja Usipime kichwa mi siwazi kama nnavyoongea Mengi yanayokukuta marafiki wanachochea Kua Misosi, tafuta pa kutokea Sio pesa, sio simu, sio gari, sio nyumba, safari utapotea [Hook] - Chozi Nimeshaona mbele, now the game is right on Kuna vikwazo tele, jasho langu halivuji bure [Repeat] [Verse 3] - Salmin swaggz Usishangae mi kukushtua yakupasa uzidishe dua Ukibisha ni sawa na white T-Shirt gizani unaifua Nakutreat, zaidi ya Piriton na magonjwa ya mafua Na hii ni kinga, tahadhari na ushauri kabla ya kuugua Tamaa itakumaliza kama mwanzo hukujua Au fanya ka kipindupindu kabla ya inzi kutua Hii ni zaidi ya mama kumtuliza mtoto akikua Together tutasmama kumkimbiza asiweze kutuua Waganga walishatabiri na watabiri wakatafsiri Hakuna atakayebaki tukiendekeza tama za mwili Dhiki imekithiri maskini hawana muhimili Wenye akili hawana dili zimebaki waadhiri na sio siri No maendeleo, ni ukoloni mamboleo Wan*lia sana jimboni ngoja wavikamate vyeo Bado kuwekwa jikoni kesho wakuite kimeo Usintazame machoni ka vipi ukapimwe leo… (Chorus) (Chozi) Nimeshaona mbele, now the game is right on Kuna vikwazo tele, jasho langu halivuji bure (Outro) There's another one, Noma Records Nicco, Kalulete, Chozi Sebuyu, Salmin *fade*