Duke Tachez - Uongo lyrics

Published

0 198 0

Duke Tachez - Uongo lyrics

Intro: Duke Tachez S.O.N.G.A Tamaduni Muzik [Verse I: Songa] Ayo karibu, kwangu ikulu ghetto Obama kanicheki, anataka ni zuru kesho Niende pande za huko, niondoe mshtuko Ana wasiwasi, Osama yuko huku keko Huh, hii ni hatari bro Wala siende, ngoja nipitishe chai kwa koo Pembeni mapokopoko, makulaji Chapati kubwa kama round about ya kariakoo Wanauliza vipi eti Wamesahau kama, huwa nakula msosi wenye nembo ya TBS Ni kama nina undugu na pesa Haki ya Mungu, waweza pata uchungu kwa presha Wazungu wanakesha Wanipige juju, wanachekesha ni ka kukuta mzuzu kwa Texas Na wala sio uzushi kwa street Muulize Duke, mi huwa naingia boothe na kiti Hook: [Nasema Uongo, ili Uongo uwe kweli Uongo Na ukiwa Uongo, ni kweli Uongo] x4 [Verse II: Songa] Nailipa sirikali Na tambua nahusika, kila usikiapo dili kali Rasilimali, na miliki nasambaza huduma clear Kama nina digitali Usitake ni kimbia, nna pesa Nime ajiri majambazi ili waje kuniibia Umaskini bye bye Nagawa connection, hata kama una wi-fi Michuzi ninayo, wapuuzi ambao Wanajifanya Gangsters Wanatembea na mbwa mi huwa natembea na mbuzi kibao Na bado sija-loose mafao Nikiwa club, mitungi, si dundi Na kama unapita unapunga, si pungi Usiumize sana kichwa kama una __ kwa ubongo Tambua tu huu ni uongo Hook: [Nasema Uongo, ili Uongo uwe kweli Uongo Na ukiwa Uongo, ni kweli Uongo] x8