Duke Tachez - Niite Songa lyrics

Published

0 799 0

Duke Tachez - Niite Songa lyrics

[Intro] Yeaah… Duke Tachez.. yeeah [Ubeti wa Kwanza] Yeah, kwa uzima nafungua kinywa nach*moa hii habari Naisoma kwa kina vina vinatoboa ka' bikari Nimepima homa kwenye roho ya hii sayari Wanasema n'na ngoma eti nakohoa mistari Sihitaji support kupost stanza nia Verse ni lugha mbili ka' noti ya Tanzania Vibaraka wana njaa, bosi anawaza mia Ni mkosi balaa, kitaa tozi anatanga njia Mbwiga hasifiki kwa ubingwa wa busara Ukiona giza na jogoo haliwiki ujue mida ya kulala MC vipi? Mbona huwakilishi shida ya fukara? Au umeshapata tija umesahau tiba uchwara? Mdomo… hauachi tathmini ya amani ya mswaki Mtoa roho angepokea rushwa maskini gani angebaki? Stuck kwenye move mi' ni mkali kwenye flow Na-scratch maujuzi m' ni chaki we ni black wall Mzungu anaiga kwenye shida ndugu Mungu Narusha machungu zaidi ya miba ya nungunungu Nyoa dungu huu ni msiba mbwiga tubu Nimeshika rungu nyumbu anasinywa ka' sungusungu! [Kiitikio x2] Niite SONGA! Kanuni ya harakati Wana haraka wapo kati nabuni sina tamati Niite SONGA! Thamani ya muwajibikaji Maisha darasa huru na mi' ndo muelimikaji [Ubeti wa Pili] Wazazi wanasema nimeshakua Ina maana… vibaya na vyema nimeshajua Jua linazama tazama inanyesha mvua Nakesha kwa dua kumuombea anayekesha akivua Alfajiri inafika na mwezi unazama Jogoo la Mbishi lawika na wezi wanahama Yamaanisha zienzi tenzi kwa ujenzi salama Uweze chutama japo kuna washenzi wanabana Wanasema mi' ni mkali ila why sisikiki? Bei ya sukari inafanya ninywe chai na pipi Rafiki… mnafiki hanifai kwa dhiki N'nachomshukuru Mungu tu uhai silipii Cheza pazuri, ukiweza eneza kauli Wajinga wanatoa macho ka' wamepoteza nauli Tenzi shule kwa hizi tungo nikumbuke Hizi verse nagawa bure kwenye midundo ya Duke [Kiitikio x2] [Ubeti wa Tatu] Baba ananiambia… Maneno hayavunji kuti Sawa nachana ila mbona flow zangu hazifumi suti Mi' mweusi roho yangu haifugi chuki Dada anasema usiposoma mdogo wangu utarudi bushi Meza ukweli kwa pressure uteme uongo Palla anasema Mhaya nd'o kauleta umeme bongo Kama husajiliwi jitahidi uchenze ndondo Mwema Mungu sio Said anayesema ubebe gongo Sifuri ndio inaanza na moja ndio ya pili Cha ajabu ya pili inaanza na kwanza inasubiri Hoja ya kishamba haina haja ya kuijadili Hii ni hoja ya kijanja pata stanza na akili Hii mic ni shamba na mimi ndio mkulima Navuna ninachopanda na ulimi ndio unalima Hapa utaganda huu sio Umwinyi na Ujima Mzazi mwambie mwana mjini si pa kupima… [Kiitikio x2]